NAOMBA BARAKA
Auteur : J.M Salisali
Usage : Méditation,

NAOMBA BARAKA

R/ Kama ulivyo wingi 
Wa nyota za angani, 
Ninaomba Bwana 
Uya jaze baraka maisha yangu 

Neema zinitiririkiye, 
Neema zinitiririkiye
Naomba furaha yako Bwana, 
Naomba faraja yako Bwana, 
Ninaomba Bwana 
Uyajaze baraka maisha yangu

1.  Kama ile baraka uliomjalia, 
Baba yetu mtumishi wako Abrahamu, 
Mfano wa nyota zaanga, 
Mithili ya mchanga wa pwani 
Naomba nijalie na mimi baraka.

2.  Na kama yakobo na uzao 
wake wote,
Baraka zako ulimjaza kwa upendo, 
Maana wewe unaweza na nguvu, 
Asili ya vyote 
Naomba nijalie na mimi baraka 

3. Unijaze nguvu na akili kiimani, 
Naitaji mwanga na mwongozo 
wako Mungu, 
Daima une nami e Bwana 
Milele, nikufuate wewe, 
Naomba nijalie na mimi Baraka

Partition

Télécharger la partition

Audio