Auteur :
Marius Nshombo
Usage :
Carême, Vendredi Saint, Sacréments,
1.
Wote walio uona msalaba wa Yesu
Walibadilika maisha na tabiya
Hauwezi pita pembeni ya musalaba
Tena ukabaki vile ulivyo kuwa
Mambo mengi sasa yatabadilika
Maishani mwako ukimwona Yesu
Refrain :
Musalaba wake Yesu
Chemchem ya neema
Kakubali kufariki (ili)
Wewe nami tuokoke
Hilo fumbo la imani
Siwezi kulisahau
Kwake Yesu ni mateso
Kwetu sisi ni wokovu
Kakubali kuteseka (ili)
Wewe nami tuokoke
Hilo fumbo la imani,
Sherti nikalitangaze eee
2.
Mitume wa Yesu na wote waliyo mfwata
Waliacha vyote na kumuzingatiya
Wengi kati yao waliteswa nakuuwawa
Ila maishani mwao furaha na furaha
Ukibeba musalaba mpaka mwisho,
Ukikufa naye utafufuka naye.