
Shirika la Kristu simameni tukaribiye meza ametayarisha Bwana, Wakristu wa Mungu tusogeye Twende tule chakula, chakula cha uzima. 1. Mukate na divayi Tunavyovipokeya Mwili na damu yake Mwokozi Bwana Yesu Tumepewa na Kristu Mwili na damu yake Ili tuishi naye Leo na siku zote. 2. Kristu aliye kuwa Mwana wa Mungu Baba Akashuka duniya akawa mwana damu Kwa zambi zetu sisi, Akaitowa mwili Mpaka akafariki Ili tuokolewe 3. Hakuna na upendo Unaopita ule Wakujitowa lote Hata mpaka na kufa Tunaposherekeya Mwili na damu yake Tunakumbuka huo Upendo kamilifu