BWANA NI MWANGA NA WOKOVU
Auteur : Baudoin Mihigo
Usage : Méditation, Engagement, Sacréments, Psaume 26,

BWANA NI MWANGA NA WOKOVU

R/ Bwana ni mwanga 
na wokovu wangu
Nimwogope nani
Yeye ukingo 
wa uzima wangu
Nitetemeke mbele ya nani

1. Wanaponishambuliya 
watu wabaya
Kwa kupoteza 
uzima wangu
Wanateleza na kuanguka

2. Adui zangu wakipita 
kwangu mimi
Moyo wangu 
hautaogopa
Maana naamini Mungu wangu

(3. Na jambo moja ninalomuomba Bwana,
na hilo kweli ninalatamani,
nikae siku zote za maisha yangu,
nifurahiwe na hekalu lake.

4. Anayenificha katika banda lake,
siku zote katika hatari, atanikinga
kabisa hemani mwake, ataniinua
juu ya mwamba.

5. Naamini kuona wema wake Bwana,
katika inchi ile ya wazima,
umtumainie Bwana uwe hodari,
ujipe moyo umtumainie.

6. Bwana ni mwanga wangu,
na wokovu wangu, wokovu wangu nimwogope
nani, yeye ukingo wa uzima wangu,
nitetemeke mbele ya nani?)

Partition

Télécharger la partition

Audio