Auteur :
Huberto Buse Meluma
Usage :
Sacréments, Christ-Roi,
Twakushukuru twakusifu
Ee Mungu wetu:
Kwako Mungu sifa yetu,
Kwako baba wa Milele
Wimbo wa ulimwengu.
Malaika wakuu
(wanapiga magoti)
Wanapiga magoti
Mbele yako Mungu baba
Mbele Yako Bwana.
Pia malaika (wanapiga magoti )
Na mizimu ya mbingu
Mbele yako Mungu baba
Mbele Yako Bwana.
Wote wanakushukuru
Bwana Mungu ee,
Wote wanakuabudu
Bwana Mungu ee,
Wanakuimbiya
Mtakatifu uh,
Mtakatifu uh,
Mtakatifu uhu,
Bwana Mungu wa ulimwengu
Mbingu na dunia zimejaa
Sifa yako.
Mitume wanakusifu,
(E Bwana)
Manabii wanakutangaza,
(E Bwana)
Mashahidi wanakushujudu,
(E Bwana)
Eklezia ina kuhubiri na kukutambua
Popote duniani.
R/ Mungu tunakuabudu
Baba mtakatifu sana,
Mwana mpenzi na wa milele
Roho ya nguvu na ya amani.
Kristu mwana wa Mungu mzima a
Bwana wa sifa a,
Kristu haukuogopa kutwaa mwili ii
Katika mwili wa bikira,
Kristu kwaku wakomboa watu uu
Utumwani mwa Zambi. R/
Kwa ushindi wako
juu ya kifo ee Bwana,
Uliwafungulia
watu njia ya ufalme,
Unatawala
kuume kwa baba,
Utarudi kuwa amua
wazima na wafu. R/
Ujionyeshe kuwa mkinga
na rafiki ya watu
walio kombolewa na damu yako. R/
Uwatwae wote pamoja
Na watakatifu wote
Katika furaha
Na mwanga wako
Amen amen amen amen