JENGA URAFIKI NA YESU
Auteur : Sindani P.T.K.
Usage : Méditation, Eucharistie, Mission, Engagement, Sacréments,

JENGA URAFIKI NA YESU

R/ Jenga urafiki na Mwokozi Yesu
Amana ya Mbingu kurithishwa
Tembea na yeye upendavyo
safiri na yeye uwezavyo
Kula na yeye popote pale

1. Anza basi leo kuwa na yeye
Rafiki wa kweli katika Mbingu 
Usichelewe kuwa na yeye

2. Ni kinga kamili ukiwa naye
Kwa taabu zako popote pale,
Anayajua maisha yako

3. Kwa magonjwa yako ndiye tabibu
Ayajua yote magonjwa yako
Ongozana naye utapona

4. Jibu la maisha ukiwa naye
Anapokuwapo hana mpinzani
Jipendekeze unufaike

Partition

Télécharger la partition

Audio