WEWE NDIWE PETRO
Auteur : Marcellin Mugenza
Usage : Méditation,

WEWE NDIWE PETRO

R/ Wewe ndiwe Petro
Maana yake mwamba
Na juu ya mwamba huo
Nitajenga Eklezya yangu
(Wala nguvu)
Wala nguvu za mauti hazitaishinda

1. Nitakupa wewe funguo
Za ufalme wa mbingu
Lolote utakalofunga duniani
Litakuwa limefungwa mbinguni
Na lolote utakalofungua duniani
Litakuwa limefunguliwa mbinguni

2. Nimekuweka wewe mkuu
Wa Eklezya
Nakuamuru uzilinde kondoo zangu
Uziongoze katika ukweli
Utangaze nono langu duniani kote
Ili mataifa wapate wokovu

Partition

Télécharger la partition