
Ave, ave Maria Ave, ave Maria mama 1. Mama Maria Mama wa huruma Musaada wetu Na muombezi wetu mama. 2. Mama Maria Utupokeleye Sisi wana wako Tunakukimbiliya mama 3. Mama Maria Utuangaziye, Gizani tulimo Utuleteye mwanga mama 4. Mama Maria Tufundishe nasi Kumujibu Mungu, Tuseme nasi ndiyo mama 5. Mama Maria Sisi wenye zambi, Tuonyeshe njia Tufate njia nzuri mama