FURAHA KATIKA KRISTU
Auteur : Marius Nshombo
Usage : Méditation, Action de grâce, Mission, Engagement, Sacréments,

FURAHA KATIKA KRISTU

1. Furaha ninayo katika kristu, 
Ni furaha bila mwisho
Mapendo alinionesha yesu, 
Mapendo bila mipaka 
Maishani mwangu mwote 
Nimeona mkono wake
Bado tumboni mwa mama
Aliita jina langu
Na tangu kuzaliwa kwangu 
Bado haja niachiliya
Wakati ninapoishi 
Ninaishi naye kristu 
Ninaishi kwa furaha
Mimi nitakapo kufa 
Nifariki naye kristu

R/  Nitazingatiya kristu 
maishani mwangu 
Na sitamuacha kamwe, 
na sitamuacha kamwe 
Kweli nitaishi na Yesu 
maishani mwangu 
Na nitaongozwa naye 
na sitamuacha tena

2. Kuishi kikristu kwa mwanadamu 
Si kwepesi nimeona 
Dunia tunayo ishi kwa leo  
Popote ni vishawishi
Pasipo neema ya kristu 
Ningeishi namna gani 
Mwili wangu ni mzaifu 
Ila kristu yupo nami 
Nikipita njiya za giza 
Kristu huniangaziya 
Wakati natenda zambi 
Nikimuomba huruma 
Zambi zinasamehewa 
Maishani mwangu mwote 
Yesu kristu yupo nami

Partition

Télécharger la partition

Audio