
R/ Simama, simama imara, jilinde Lilinde, neno lako Bwana imara Kesha kila siku uombe, (uombe) utasimama 1. Milima yote na mabonde itayeyuka Neno lake Bwana imara, (imara) –litasimama 2. Mapendo ya Mungu, tumejaa roho ya kweli Imara yetu ndani yake, (ndaniye), awe muhuri 3. Siku za huduma ni chache, tuwe mashujaa Roho wa Yesu akaa nasi, (kaa nasi) mpaka hatima 4. Katika yote tutashinda, kwa nguvu yake Nani aweza kututenga, (kutenga), na pendo lake 5. Heri ashikaye maneno, ya Mungu Mwana Naam naja upesi Amina, (amina) njoo Yesu Bwana